Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya

Kenya Airports Authority
AinaKiserikali
SektaUsafiri
BidhaaHuduma na Shughuli katika Uwanja wa Ndege
Tovutihttp://www.kenyaairports.co.ke

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya (kwa Kiingereza: Kenya Airports Authority: kifupi: KAA) ni taasisi inayomiliki viwanja tisa vya ndege nchini Kenya. Inahusika pia kutoa vibali kwa viwanja vya ndege vya binafsi.

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Kenya ilianzishwa kwa sheria ya bunge katika mwaka wa 1992. Sheria hiyo ya KAA Act, kifungu cha 395, hueleza nguvu na utendaji wa mamlaka.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne